Ili kuonyesha mshikamano wa kitaifa kwa familia ya marehemu, viongozi mbalimbali, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, walifika nyumbani kwa familia Bweleo, Mkoa wa Mjini Magharibi, kutoa pole na faraja.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Zanzibar, (jana) 25 Septemba 2025 - Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amepokea mkono wa pole kufuatia kifo cha kaka yake, Abbas Ali Mwinyi, kilichotokea jana.
Ili kuonyesha mshikamano wa kitaifa kwa familia ya marehemu, viongozi mbalimbali, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, walifika nyumbani kwa familia Bweleo, Mkoa wa Mjini Magharibi, kutoa pole na faraja.
Miongoni mwa viongozi walioungana na Rais Samia ni:
1_ Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Mashaka Biteko
2_Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu
3_Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla
4_Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zuberi Ali Maulid
5_Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro
6_Pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali.
Tarifa ya mazishi:
Marehemu Abbas Ali Mwinyi atasaliwa Masjid Jamia Zinjibar, Mazizini baada ya Sala ya Ijumaa, na kuzikwa Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, leo tarehe 26 Septemba 2025.
Your Comment